Billionaire wa England Jim Ratcliffe (71) ataanza haraka kuiongoza klabu ya Manchester United mara baada ya Familia ya Glazer itakapoachia ngazi.
Tayari tajiri huyo ameanza mipango ya namna ya kuiendesha klabu ya Manchester United iwapo dili la kununua hisa ndani ya klabu hiyo litakamilika, Ratcliffe anataka kuanza kufanya maboresho kwenye eneo la kutafuta vipaji, kwa maana hiyo kibarua cha Mtendaji mkuu Richard Arnold, na mkurugenzi wa soka John Murtough na David Harrison kipo mashakani. Harrison aliteuliwa mwezi wa Pili kushika hatamu hiyo.
Ratcliffe anashangazwa na utendaji kazi wa watendaji hao kwa matumizi makubwa ya pesa tangu kuondoka kwa aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward.
Kwa misimu kadhaa tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, Manchester United imetumia takribani Billion £1.4 kwaajili ya usajili wa wachezaji. Kwa kipindi hicho maafisa hao wa Manchester United wamenunua wachezaji wasio na viwango wengi.
Hii inahusisha sajili zilizovunja rekodi za usajili wa klabu hiyo ikiwemo usajili wa Paul Pogba £89m, Antony £85.5m, Romelu Lukaku £75m, Jadon Sancho £73m, Angel Di Maria £59.7m, Anthony Martial £44.5m, na usajili wa Donny van de Beek uliogharimu £35m.
Licha ya kufanya usajili huo Manchester United haijawahi kubeba makombe makubwa tangu mwaka 2013, wakibeba FA Cup moja (1), makombe ya Ligi mawili (2) na Europa League moja (1) tangu Sir. Alex Ferguson aliposhinda mataji 28.
Erik Ten Hag ametumia £374m tangu amechukua kikosi hicho, lakini Ratcliffe anamkubali zaidi Erik kwasababu alimaliza nafasi ya tatu (3) na mafanikio aliyoyapata kwenye michuano ya Carabao Cup, hii ina maana huenda Erik akaendelea kusalia chini ya umiliki wa Ratcliffe.