CAF Women Champions League

SHIME: JKT ITAFUZU NA WACHEZAJI WALIOBAKI.

Published on

Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa upande wa Wanawake inaendelea kesho kwa michezo ya mwisho ya hatua ya makundi kuchezwa. JKT Queens kutoka kundi A mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki itashuka dimbani kuikabili CS Casablanca ya Morocco majira ya saa tano usiku (23:00) kesho, Jumamosi, November 11.

Kuelekea katika mchezo huo baadhi ya nyota wa klabu hiyo wameondoka nchini Ivory Coast kurejea nchini Tanzania hii leo, kwaajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 inayojiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya timu ya Taifa ya Nigeria, mchezo utakaopigwa Jumapili katika dimba la Azam Complex Jijini Dar Es Salaam.

kufuatia kurejea nyota hao nchini licha ya kuwa na mchezo mzito na mhimu kwa JKT Queens dhidi ya CS Casablanca, watanzania na wapenda soka wamekuwa na maswali mengi wakijiuliza hili limewezakana vipi.

Daudasports imefanya mahojiano na kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania, chini ya miaka 20, Bakari shime kuhusu hili limewezekanaje kufanyika.

Bakari amesema hakuna tatizo kwa wachezaji wa klabu ya JKT Tanzania kuondoka kambini nchini Ivory Coast kuja kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania licha ya kuwa na mchezo mhimu hapo kesho kwani wachezaji waliobaki wanauwezo wa kuipatia matokeo timu hiyo na kufuzu nusu fainali.

Hakutaathiri kitu kwasababu jambo hili sio la kushtukiza kwenye benchi la ufundi, TFF kwa upande wake wameandika barua kuwaomba CAF kuwaelezea hili na CAF hawakulipa uzito.

Sisi kama watu wa ufundi tulijiandaa kuona kwamba kuna wakati utafika, JKT itakuja kucheza bila wachezaji hao ambao watatakiwa kucheza kwenye majukumu ya timu ya Taifa, kwetu sisi sio jambo la kushtukiza na tumeshajipanga nalo.

Panapo majaaliwa mara baada ya mchezo huu [wa Taifa] wataondoka tena kurejea Ivory Coast kwaajili ya kucheza nusu fainali kwasababu tunaamini wachezaji waliobaki watafanya vizuri kwenye mchezo ujao.

Sio kwamba wachezaji hao hawana umuhimu kwenye kikosi cha JKT Queens, kwamfano mechi ya kwanza wachezaji wote hao walikuwepo kwenye mashindano na JKT ilipoteza mchezo, mechi ya pili juzi imechezwa wakashinda ni wachezaji watatu ambao hawatakuepo kwenye mchezo ujao.

Sio kwamba JKT haiwezi kufanya vizuri bila hawa, na si kwamba JKT haiwezi kupoteza bila hawa, ndio maana hawa wote walikuwepo Ivory Coast na mchezo wa kwanza tumefungwa,

Bakari Shime, Kocha wa timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 na mshauri wa benchi la ufundi la JKT Queens.

JKT Queens ina kibarua kesho dhidi ya CS Casablanca, huu ni mchezo wa mwisho wa kukamilisha michezo ya hatua ya makundi endapo itashinda itaungana na Mamelodi Sundowns Ladies ambao tayari wamefuzu.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake chini ya miaka 20 itashuka dimbani saa 9:00 Alasiri katika dimba la Azam Complex Chamazi Dar Es Salaam Jumapili hii ya November 12.

https://daudasports.co.tz/wp-content/uploads/2023/11/SHIME.mp3

Popular Posts

Exit mobile version