Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20 [Tanzanite] hii leo imetoshana nguvu na timu ya Taifa ya Wanawake ya Nigeria kwa kufungana goli 1-1 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, Jijini Dar Es Salaam. Goli la Tanzanite limefungwa na Asnath Ubamba huku goli la Nigeria likiwekwa kimiani na Chioma Olise.
Huu ni mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa umri chini ya miaka 20, mchezo wa marejeano utapigwa nchini Nigeria siku chache zijazo. Kwa matokeo haya Tanzanite ina kibarua kizito cha kwenda kupata matokeo ugenini nchini Nigeria, ili ifuzu kwenda hatua inayofuata.