Kocha mkuu wa kikosi cha Wydad AC Adil Ramzi anaamini Mamelodi Sundowns wamepata uzoefu wa kutosha kuhusu zoezi la upotezaji wa muda kwenye michuano ya African Football League.
Wydad AC walionekana wakilaumu baada ya dakika 90 kumalizika kutokana na mwamuzi kuonyesha dakika tano pekee, wakiamini zilitakiwa kuongezwa zaidi ya hizo tano kwasababu Mamelodi Sundowns walipoteza sana muda katika wakati wakiongoza 3-2 kwenye dimba la Loftus Versfeld.
Hii inatafsiriwa kama sababu ndogo sana ya timu yake ya Wydad AC kupoteza mchezo huo na pia ameonyesha kutokuliheshimu soka la Mamelodi Sundowns ambalo wamelionyesha tangu kuanza kwa Ligi hii ya African Football League.
Nilisema baada ya mchezo wa kwanza pale Casablanca, niliona mpira unachezwa kwa asilimia 100, kwahiyo naheshimu namna wanavyocheza lakini tunajua kwenye mpira na kwenye mpira wa hali ya juu kwasababu matokeo ni mhimu.
Ramzi alisema baada ya kuulizwa kuhusu upotezaji wa muda.
Lakini sisemi [Wachezaji] lazima wawe waigizaji, nafikiri Sundowns, kwasasa wana-uzoefu zaidi kuliko miaka iliyopita. Kwetu sisi, naweza kuielezea timu yangu, najivunia timu yangu na tumepoteza sio kwamba hatukuwa na mipango bali ni matatizo ya utimamu.
Kama tungekuwa vizuri tungekuwa na nafasi nzuri ya kupata matokeo lakini sawa, wanastahili, wameshinda, tunatumaini pamoja tunaweza kujaribu na kuwapa mashabiki wetu mpira mkubwa kwa Afrika.
Adil Ramzi aliongeza, baada ya kupoteza mchezo wa pili wa fainali wa African Football League.