Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imefikia mzunguko wa tisa (9) kwa kila timu kucheza michezo tisa (9) isipokuwa Simba na Mashujaa ambazo zimecheza michezo nane (8) pekee.
Hadi kufikia hivi sasa mshambuliaji wa Simba Jean Othos Baleke amepiga mashuti tisa [9] katika mechi Saba [7] za ligi kuu alizocheza mpaka sasa msimu huu. Saba [7] yalilenga lango na mawilii [2] hayakulenga lango.
Amefunga magoli Saba [7] na kutoa pasi moja [1] ya goli.