Makala Nyingine

SIMBA SC YAZINDUA WHATSAPP CHANNEL.

Published on

Klabu ya Simba leo hii imezindua Simba SC Whatsapp channel, kwaajili ya kutoka taarifa Kwa Mashabiki wa Simba duniani kote. Akizungumza na waandishi wa habari CEO wa klabu ya Simba Imani Kajula amesema channel hii itakwenda kuongeza urahisi wa kupata habari za klabu.

Simba imekua klabu ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwa na chaneli maalum ya WhatsApp ambayo itawapa habari mashabiki na wabia wake. Ikiwa inaingoza kwenye mitandao ya jamii, hii ni hatua kubwa kwani zaidi ya watu 2.7 Bilioni wanataumia WhatsApp hivyo Simba itakuwa karibu zaidi ya mashabiki wake na pia kuwa chanzo kizuri cha kuongeza thamani kwa wadhamini wake na wabia wengine.

Alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Iman Kajula.

Sambamba na hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba SC alisema kuwa ni timu tatu pekee barani Afrika zilizofungua whatsapp Channel ambazo ni Al Ahly ya Misri, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Simba SC ya Tanzania.

Ni timu chache kama Kaizer Chiefs, Al Ahly, Barcelona, Real Madrid na Simba tumejiunga. Katika kuijaribu kabla ya kuzindua ndani ya wiki tumepata wafuasi laki moja. Faida kubwa ni mashabiki kupata taarifa na wadhamini wetu kuonyesha bidhaa zao.

Aliongeza Iman Kajula.

Aidha, mtendaji huyo wa Wekundu wa Msimbazi Simba SC alisema ujio wa channel hiyo unakuja na jaira ya mtu kwa maana kwamba kutakuwa na muajiriwa mpya atakaye husika na nafasi hiyo.

Ujio wa Simba WhatsApp Channel unakuja na ajira kwa mtu maalumu kuwa na kazi ya kutoa habari.

Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo alimaliza kwa kusema hivyo.

Popular Posts

Exit mobile version