CAF Champions League

SVEN AITAJA MAMELODI TIMU BORA AFRIKA.

Published on

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, CR Belouizdad na Wydad AC, Sven Vandenbroeck ameitaja klabu ya Mamelodi Sundowns kama timu yake bora na ambayo hajawahi kuiona Barani Afrika kwa namna timu hiyo inacheza kwa uwezo wa hali ya juu.

Mamelodi Sundowns ilikuwa timu yangu bora msimu uliopita, ilistahili kubeba ubingwa wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika [Msimu uliopita]. Sijawahi kuona timu inayocheza kwa ubora ule kwenye hili Bara la Afrika.

Sven Vandenbroeck.

Sven alikutana na Mamelodi Sundowns akiwa na Wydad AC msimu uliopita katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika na kuiondosha klabu hiyo kwa faida ya goli la ugenini baada ya matokeo ya jumla kumalizika kwa sare ya 2-2 waliyoipata katika dimba la Loftus Versfeld, Pretoria, Afrika Kusini.

Hata hivyo Wydad AC ilipoteza mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika mbele ya Al Ahly waliokuwa mabingwa kwa msimu huo. Baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi minne Sven aliondoka klabuni hapo na kuelekea CR Belouizdad ya Algeria

Popular Posts

Exit mobile version