Cyprus wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa kama vibonde wa kundi A wakipoteza michezo yote huku wakifunga bao 1 tu na kuruhusu mbao 20 langoni mwao.
Spain wenyewe ndio vinara wa kundi wakiwa na alama 15 sawa na Scotland na wanahitaji sana ushindi wa leo ili kuendelea kujiweka kileleni na wanaamini kwenye kuifunga mabao mengi zaidi Cyprus kutaendelea kuwaweka kileleni.
Spain ameshafunga mabao 16 mpaka sasa na wana safu nzuri ya ulinzi wakiruhusu 1 tu kwenye michezo 5 iliyopita.
DONDOO : USHINDI NA MAGOLI ZAIDI YA 2.5 KWA SPAIN
Wakiwa hawajashinda hata mechi 1 kwenye mechi zao 5 za mwisho na wakitoka kunyukwa 4-0 na Iceland, ni wazi hawatokuwa na mechi nyepesi dhidi ya wababe Ureno ambayo waliwachapa 5-0 Bosnia & Herzegovina kwenye mechi yao ya mwisho.
Ureno washapachika mabao 19 kwenye mechi zao 5 za mwisho, wastani wa karibu mabao 4 kwa mechi moja na ni mechi 1 tu kati ya hizo wameshinda wakiruhusu goli yani GG. Bila shaka Cristiano Ronaldo atataka kuendelea kuvunja rekodi zake.
DONDOO : USHINDI NA MAGOLI ZAIDI YA 2.5 KWA URENO
Wanapokutana Cape Verde na Angola tayari inakuwa ni vita kubwa kutokana na sababu nyingi lakini kubwa zaidi timu zote zina wachezaji wengi wazuri na wenye asili ya Kireno.
Cape Verde walifungwa 2-1 kwenye mchezo wao wa mwisho na Comoros huku Angola wakitoka 0-0 dhidi ya Congo DR. Cape Verde wakishinda mechi 1, sare 1 na Kufungwa michezo 3 huku Angola akifungwa mechi 1, akitoa sare 3 na kushinda 1 kwenye mechi zao 5 za mwisho.
Magoli huwa ni machache baina yao. Lakini Kufungana inawezekana kwakuwa wote wanapenda kucheza na wanafunga na kufungwa pia.
DONDOO : MAGOLI CHINI YA 3.5 AU TIMU ZOTE KUFUNGANA