Michuano ya Cecafa U15 imetamatika hii leo kwa mchezo wa fainali kufanyika kati ya Uganda na Zanzibar, na Zanzibar kuibuka mabingwa wa michuano hii.
Zanzibar imeibuka Bingwa kwa kuifunga Uganda kwa changamoto ya mikwaju ya Penalty 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizi kutoshana nguvu ya kufungana goli 1-1.
Tanzania imeshika nafasi ya Tatu ya mashindano haya baada ya kuifunga Sudan Kusini goli 1-0 kwenye mchezo wa mapema hii leo.
Tuzo zilizotolewa
Golikipa bora wa mashindano – Faki Abdallah (Zanzibar)
Mfungaji bora – Lazaro Peter George (Ethiopia)
Mchezaji bora – Owen Mukisa (Uganda)
Zanzibar – Bingwa.
Uganda – Mshindi wa Pili.
Tanzania – Mshindi wa Tatu.