Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania

TANZANITE KUIKABILI NIGERIA JUMAPILI.

Published on

Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ ipo nchini Nigeria kwaajili ya mchezo wa marejeano wa kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Timu ya Taifa ya Nigeria. Mchezo wa kwanza wa timu hizi mbili ulipigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi, Dar Es Salaam ulimalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.

Tanzanite imeelekea nchini Nigeria ikijua kuwa matokeo ya kwanza waliyoyapata sio rafiki kwa upande wao na hivyo watalazimika kupata ushindi au sare ya kuanzia magoli mawili ili waweze kusonga kwenda hatua inayofuata.

Tumekuja hapa tukiamini tunakuja kupambania kutafuta nafasi ya kusonga mbele, matokeo tukiwa tunayafahamu kuwa tuko nyuma, ni sare ya magoli ama kushinda ndipo tutapata nafasi ya kusonga mbele.

Bakari Shime kocha wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake U20 akizungumza kuelekea mchezo wa Jumapili.

Popular Posts

Exit mobile version