Chelsea

OBI MIKEL: MESSI WA SAYARI NYINGINE.

Published on

Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Nigeria, John Obi Mikel ameeleza kuwa kipindi akiwa Chelsea walikuwa wanamwachia Ashley Cole kazi ya kumkaba Cristiano Ronaldo kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Manchester United, lakini kipindi wakiwa wanaenda kukutana na Barcelona walikuwa wanafanya mazoezi wiki nzima ya namna ya kumkaba Messi.

Tulipokuwa tukicheza dhidi ya Manchester United, tulijua Ashley Cole atamdhibiti Cristiano Ronaldo.

Lakini mara zote tulipocheza dhidi ya Barcelona, mazoezi ya wiki nzima yalikuwa namna ya kumdhibiti Messi

Wachezaji wawili hadi watatu wakitakiwa kutembea naye. Huwezi kujilinda mmoja kwa mmoja dhidi ya Messi… haiwezekani.

Kwangu mimi, sioni kabisa cha kulinganisha. Messi wa sayari nyingine.

John Obi Mikel kuhusu Leonel Messi na Ronaldo, Chelsea FC 2006 – 2017.

Baada ya maneno hayo, Mwana habari mkongwe nchini Tanzania Thabit Zakaria akaja na takwimu za michezo ya Chelsea yenye John Obi Mikel dhidi ya Manchester United yenye Leonel Messi na Manchester United yenye Cristiano Ronaldo.

Turudi kwenye namba.

  1. CHELSEA VS MESSI

Oktoba 18, 2006
Chelsea 1-0 Barcelona
-Drogba

Oktoba 31, 2006
Barcelona 2-2 Chelsea
-Deco -Lampard
-Gudjonhson -Drogba

Aprili 28, 2009
Barcelona 0-0 Chelsea

Mei 6, 2009
Chelsea 1-1 Barcelona
-Essien -Iniesta

Aprili 18, 2012
Chelsea 1-0 Barcelona
-Drogba

Aprili 24, 2012
Barcelona 2-2 Chelsea
-Buisquets -Ramires
-Iniesta -Torres

  1. CHELSEA VS CRISTIANO RONALDO

26/11/2006
Man U 1-1 Chelsea
-Saha -Carvalho

19/05/2007 – fainali ya FA
Chelsea 1-0 Man U
-Drogba

23/09/2007
Man U 2-0 Chelsea
-Tevez
-Saha

05/08/2008 – ngao ya jamii
Chelsea 1-1 Man U (penati 0-3)
-Malouda -Giggs

26/04/2008
Chelsea 2-1 Man U
-Ballack -Wayne Rooney
-Ballack

21/05/2008 – fainali ligi ya mabingwa
Man U 1-1 Chelsea (penati 5-4)
-Ronaldo -Lampard

21/09/2008
Chelsea 1-1 Man U
-Kalou -Park

11/01/2009
Man U 3-0 Chelsea
-Vidic
-Rooney
-Berbatov

Katika kipindi cha miaka 11 cha John Mikel Obi kuichezea Chelsea, alikutana na Messi mara 6. Mara zote ni kwenye ligi ya mabingwa , na Messi hakuwahi kufunga.

Labda ile mbinu ya kumuwekea walinzi wengi ililipa.

Lakini Cristiano Ronaldo alikutana na Chelsea mara 8, kwenye mashindano manne tofauti.

Ligi Kuu – 5
Ngao ya Jamii – 1
Kombe la FA – 1
Ligi ya Mabingwa – 1

Alifunga bao moja kwenye ligi ya mabingwa

Popular Posts

Exit mobile version