Mdhamini na Mfadhili wa klabu ya Young Africans Gharibu Said Mohammed (GSM) katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa hii leo amefanya hafla fupi ya kusherehekea pamoja na wagonjwa wa saratani kwenye hospitali ya Ocean Road.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Mh. Albert Chalamila, GSM amechangia vifaa tiba vya Saratani vyenye thamani ya Million 137.
Gharib Said Mohamed amechangia vifaa tiba vya ugonjwa wa saratani kwenye hospital ya Ocean Road vyenye thamani ya Million 137.
Wazo hili lililetwa na mke wake na hii inathibitisha mafanikio siku zote yanaanza na mke wako.
Mafanikio ya klabu ya Yanga SC kwa zaidi ya asilimia 80 yamechangiwa na uwepo na Ghalib Said Mohamed. Tunamshukuru sana GSM yeye pamoja na familia yake. Ametutoa mbali sana na tunaendelea kumsihi aendelee kuinga mkono klabu hii. Nasi tutamuombea katika kila hatua kwenye maisha yake.
Alizungumza Eng. Hersi Said, Rais wa klabu ya Young Africans.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila amempongeza Gharib kwa moyo wake wa kujali wengine alionao licha ya ugumu wa maisha lakini pia akamuombea afya njema kwa kile alichokifanya, na kumsihi asiache kutenda matendo haya ya huruma.
Ndugu yangu GSM kwa hali ya maisha uliyofikia sasa wala huhitaji mambo mengi tena, unahitaji mambo mawili tu, uwe karibu na Mungu na pili uwe na afya njema. Haya unayofanya leo, Mungu lazima atakupa mtaji wa afya, ili uweze kusaidia wengine zaidi. Usiache kutenda matendo haya ya huruma kwa jamii.
Albert Chalamila -RC DSM
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewaomba wale wote waliobarikiwa kuwa na uchumi imara pia kuhakikisha wanafanya matendo ya huruma kwa jamii zenye uhitaji kwa kuwaasa kuwa kuna wakati mwingine pesa hupotea lakini matendo ya huruma hudumu.
GSM leo amechangia Tsh 137m kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Kansa hapa Ocean Road. Hapa tunapata ujumbe mzito sana, wakati mwingine pesa hupotea lakini matendo huruma hudumu. Wote mliobarikiwa kuwa na uchumi mzuri tuzidi kutenda matendo ya huruma kwa jamii.
Albert Chalamila – RC DSM.
Baada ya hafla hiyo Gharib Said aliulizwa kuhusu ushauri wake kwa vijana wanaopambana kutengeneza maisha yao ili wafikie kwenye uchumi wa juu, wengine wakifanikiwa na wengine wakifaulu yeye jibu lake lilikuwa ni moja na rahisi sana,
Yanga Bingwa.
Gharib Said Mohamed, Mfadhili na mdhamini wa klabu ya Yanga.