Manchester United wanatazamia dili la kumsajili Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid na wako tayari kuongeza mshahara wake mara tatu zaidi.
Ripoti zinadai kwamba kwenye mkataba wa Griezmann na klabu yake ya Atletico Madrid kuna kifungu cha kiasi £22m kinachomruhusu Mfaransa huyo kuondoka endapo atahitajika kujiunga na klabu nyingine.
Inafahamika kuwa Mfaransa huyo ana furaha ya kuitumikia Atletico Madrid, kwa hivyo United wanapaswa kufanya kufanya kazi ya ziada kukamilisha uhamisho huo. Inadaiwa Manchester United iko tayari kuongeza mshahara wa Griezmann mara tatu zaidi kutoka €7m kwa mwaka hadi €21m kwa mwaka sawa na £355,000 kwa wiki.
Pia bado haijawekwa wazi kama United itafatilia uhamisho huo katika dirisha dogo la Januari au hadi msimu wa joto utakapowadia. Lakini kama Sancho na Martial wote wataondoka kwenye dirisha la majira ya baridi, huenda usajili wa Griezmann ukakamilika mapema.