Simba

SIMBA YATAMBULISHA JEZI MPYA NA MASWALI MENGI.

Published on

Klabu ya Simba ya Tanzania leo rasmi imetambulisha jezi zake mpya itakazozitumia katika michezo yake ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu huu kuanzia hatua ya makundi. Simba imeachia jezi aina tatu, Nyeupe ambayo hutumia ugenini, nyekundu ambayo ni jezi ya nyumbani na Blue ambayo ni jezi namba tatu.

Klabu ya Simba kila mwaka imwkuwa na utaratibu wa kuzindua jezi mpya kuelekea mwanzo wa msimu wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika wakiwa na mdhamini mpya. Mdhamini wa sasa ambaye atakaa kifuani ni kampuni ya MO Extra inayomilikiwa na Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji.

Baada ya kutambulishwa kwa jezi hizo baadhi ya wadau na mashabiki wa soka wametoa maoni yao kuhusu ubora wa jezi hizo na uhalali ambao haujawekwa wazi kuhusu uwepo wa mdhamini mkuu kwenye jezi hizo kampuni ya Mo Extra.

Viongozi wanatakiwa kutoa maelezo hiyo Mo extra imeingiza kiasi gani na hiyo Mo Foundation nyuma ya jezi ni mradi wa nini mbona hauna manufaa na timu.

Halafu ni kiasi gani timu inaingiza kupitia hayo matangazo maana hii timu inaendeshwa kwa mfumo wa hisa siyo ya mtu mmoja tunahitaji ufafanuzi wa kutosha.

Shabiki mmoja wa klabu ya Simba alihoji.

Mtengeneza Jezi inabidi atafute mbunifu wa Jezi, mashabiki tunataka sana kununua na kuichangia Simba lakini karibu zote tatu za mwaka huu zinafanana na kutufanya tujiulize kwanini mtu ununue jezi mpya Kama ya Ligi inafanana na AFL na hii ya champions league???

Shabiki mwingine wa Simba Alihoji.

Mchambuzi wa kandanda nchini Farhan Kihamu naye amehoji uwepo wa udhamini wa kampuni ya Mo Extra na Mo sport kwenye jezi ya Simba uko vipi lakini pia akahitaji kujua kuhusu mkataba wa Simba na kampuni hiyo ulisainiwa lini.

Labda CEO atusaidie kidogo majibu ni kwamba hakuna Mdhamini mwingine wa kuweka hela ama? MO XTRA zipo mara mbili, juu kulia na moja kubwa mbele kifuani, kabisa hakuna brand nyingine? Jezi moja ina matangazo mawili ya kufanana?

Tajiri anatoa mzigo yes lakini hii ya kutuweka matangazo ya kufanana kwenye uzi mmoja ni kubana fursa nyingine za klabu kuingiza pesa ya kutosha kutokana na platform hii kubwa ya michuano ya kimataifa.

Halafu CEO pia atusaidie hiyo MO SPORT mkataba wake ulisainiwa lini? Ni Kampuni ya nani hii? Inajihusisha na nini hii?.

Farhan Kihamu Mchambuzi wa soka nchini.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani Jumamosi hii majira ya saa 10:00 Jioni kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya klabu ya Asec Mimosas kutoka nchini Ivory Coast.

Popular Posts

Exit mobile version