Klabu ya Singida Fountain Gate ya mkoani Singida inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara, Leo imemtangaza kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Kenya Duke Abuya kuwa mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo.
Tuzo hiyo inatolewa na Jet and Son’s Company Limited, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye klabu hiyo inasema, Duke amekidhi vigezo vilivyotumika kumchagua katika mechi zote alizocheza mwezi Oktoba, 2023.
Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni pamoja na nidhamu, msaada wake kwa timu kwenye nafasi anayocheza, mwendelezo mzuri na kucheza 85% ya mechi zote za Oktoba. Singida imecheza michezo mitano mwezi Oktoba.
vs Future [A]
vs Mtibwa [A]
vs Simba [H]
vs Namungo [A]
vs Yanga [A]
Tuzo hiyo imeambatana na kitita cha million moja [1,000,000], kiwango ambacho kilikabidhiwa na mkurugenzi wa Jet & Son’s Company Limited, Ndg. Edgar Tarimo na kupokelewa na meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Singida Fountain Gate, Hussein Massanza kwa niaba ya mchezaji.