Timu ya taifa ya Senegal imeliandikia barua Shirikisho la soka Duniani FIFA kutekeleza sheria na kuiondosha timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye fainali za kombe la Dunia chini ya miaka 17 zinazoendelea hivi sasa nchini Indonesia kwa kumtumia nyota Yanis Ali Issoufou Abdoulkadre.
Kwa mujibu wa barua hiyo inaeleza kuwa nyota huyo aliitumikia timu ya Taifa Niger wakati wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali hizo na baadae akaibukia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye fainali hizo zinazoendelea nchini Indonesia.
Senegal na Ufaransa zilikutana hatua ya 16 bora na Ufaransa ikasonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kuiondosha Senegal kwa mikwaju ya Penati 5-3 kufuatia suluhu ya 0-0 baada ya dakika tisini kumalizika. Kabla ya mchezo huo Senegal iliwasilisha malalamiko ya mchezaji huyo na mwisho wa siku Ufaransa hawakumtumia nyota huyo kwenye mchezo huo.
Kwasasa fainali hizo zimefika hatua ya robo fainali, Africa hadi hivi sasa imebakiza timu mbili pekee, Mali na Morocco ambazo zitakutana hatua ya robo fainali, timu zingine zilizofuzu hatua ya robo fainali ni Ufaransa, Uzbekistan, Brazil, Argentina, Hispania na Ujerumani.
MECHI ZIJAZO
NOVEMBER 24,2023
11:30 SPAIN vs GERMANY
UWANJA: Jakarta International
NOVEMBER 24, 2023
15:00 Brazil vs Argentina
UWANJA: Jakarta International
NOVEMBER 25, 2023
11:30 FRANCE vs UZBEKISTAN
UWANJA: Manahan Stadium [Surakarta]
NOVEMBER 25
15:00 MALI vs MOROCCO
UWANJA: Manahan Stadium [Surakarta].