NBC Premier League

MNARA WA 5G UMESOMA PIA CHAMAZI, KIPRE 3.

Published on

Azam FC imeishushia dhahma Mtibwa Sugar kwa kuwafanyia karamu ya magoli baada ya kuwanyuka mabao 5-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC na kufikisha alama 22 ikijizatiti katika nafasi ya 2 kwenye msimamo huku Kipre Jr. Akifunga “Hattrick”.

Mtibwa Sugar walionekana kuwa dhohofu tangu dakika za mwanzo kabisa za mchezo wakiiruhusu Azam kuutawala mchezo na kufika mara nyingi kwenye ngome yao.

Alikuwa ni Kipre Jr. Aliyefungua karamu hiyo ya mabao kwa kuunganisha kwa utulivu kabisa kazi nzuri ya Pascal Msindo dakika ya 18 tu ya mchezo.

Kipre Jr. Alifunga goli la pili kwake na kwa timu yake dakika chache kabla ya kwenda mapumziko safari hii akipokea pasi ya marashi ya karafuu kutoka kwa Feisal Salum “Fei Toto” dakika ya 43 na kukandamiza msumari bila ajizi.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi tena kwa Azam kuwashambulia mfululizo Mtibwa Sugar huku Makaka akijaribu kufanya wokovu mara kadhaa lakini bado timu ilionekana kuelemewa.

Dakika ya 61 ya mchezo, Azam walipata bao la 3 kupitia kwa Lusajo Mwaikenda akiunganisha kwa Kichwa krosi murua kutoka kwa Feisal Salum.

Wakati wakiendelea kujiuliza nini kimewakuta, Kipre Jr aliwatandika bao la 4 na kufunga Hattrick yake ya kwanza kwa Azam FC kwa shuti la mbali ambalo lililimshinda golikipa Mohamed Makaka ambaye alionekana kuwa ametokea golini na Kipre kummchungulia na kufunga goli zuri. Dakika ya 63, 4-0.

Zanzibar’s finest alikamilisha siku nzuri ya Azam FC leo kwa kufunga bao la 5 kwa kumalizia mpira uliopanguliwa na Makaka baada ya shuti kali la Iddy Selemani Nado kummshinda na kummdondokea Fei Toto aliyefunga “tap in”.

Mpaka dakika 90 zinatamatika, Mtibwa walikuwa wametepeteshwa kwa jumla ya mabao 5-0 na Azam FC na kuendelea kuwa Kibonde wa Azam.

Kuna mambo mengi ya kuweka sawa kwenye kikosi hiki cha Mtibwa na yanatakiwa yawekwe sawa haraka kuinusuru timu hii kongwe ambayo imepoteza kabisa ari ya kiushindani kiwanjani msimu huu.

Popular Posts

Exit mobile version