CAF Champions League

MEDEAMA KUIBANA AL AHLY LEO.

Published on

Ligi ya mabingwa Barani Afrika kundi D inaendelea kwa mchezo mmoja tena kati ya Medeama dhidi ya Al Ahly.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Medeama Evans Adotey amesema ana mbinu za namna ya kuidhibiti na kuiadhibu Al Ahly ndani ya dakika 15 za kwanza.

Nina siri kubwa kwenye mikono yangu ya kuiangamiza Al Ahly na kuhakikisha narudi nyumbani na matokeo chanya.

Evans Adotey, Kocha Medeama.

Al Ahly itakuwa na kibarua hii leo nyumbani kuialika klabu ya Medeama kutoka nchini Ghana majira ya saa nne usiku [22:00].

Al Ahly na Medeama zipo kundi moja la Ligi ya mabingwa Barani Afrika pamoja na klabu ya CRBelouizdad na Yanga.

Kinara wa kundi hilo kwasasa ni CR Belouizdad ambaye amepata ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza [3-0] dhidi ya Yanga hapo jana. Timu mbili kinara kwenye kundi hili zitafuzu hatua ya robo fainali moja kwa moja.

Michezo mingine ya Ligi ya mabingwa hii leo ni;

KUNDI B
16:00 Simba vs Asec Mimosas.
22:00 Wydad vs Jwaneng Galaxy

KUNDI C
19:00 Esperance vs Etoile du Sahel
19:00 Petro Atletico vs Al Hilal Omdurman.

Popular Posts

Exit mobile version