Bondia Mtanzania Dullah Mbabe jana amepoteza pambano mbele ya Eric Katompa kutoka nchini Congo kwa point baada ya mizunguko kumi (Round 10) kumalizika bila KO kupatikana kwenye pambano lililopewa jina la THE JUNGLE FIGHT.
Huu ni ushindi mwingine tena kwa Eric Katompa akiwa kwenye Ardhi ya Tanzania na hii inakuwa mara ya pili mfululizo kupata ushindi dhidi ya Dullah Mbabe.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa pambano la jana akasema aliingia kwenye pambano ikiwa ametoka kufiwa na mzazi wake siku moja kabla ya pambano hivyo hakuwa na nguvu jambo lililomlazima hadi kusubiri mizunguko yote imalizike ndipo ushindi upatikane.
Nimefanya mazoezi mengi zaidi, na nilikuwa najua nini nakifanya, Dullah hajabadilika ni yule yule tu, tofauti ya pambano hili na lililopita ni kwamba hili hajaanguka chini.
Nilikuwa sina nguvu sana kwasababu nimepoteza mzazi wangu jana, nimejitahidi tu niweze kupigana nae lakini nilikuwa sina nguvu.
Nimefurahi nimepata ushindi lakini nina majonzi ya kumpoteza mzazi.
Eric Katompa baada ya pambano kumalizika.
Dullah Mbabe baada ya kupoteza kwa mara nyingine tena mbele ya Katompa alidai kuwa kwenye pambano hilo alistahili kushinda na waliomfanya asishinde ni majaji kutokuthamini mabondia wa nyumbani huku akiamini chama cha ngumi nchini pengine kina ugomvi nae.
Wanachi wote naamini pambano wameliona, nimecheza vizuri, tumemalizana vizuri, Katompa yeye alikuwa anaenda hadi anataka kudondoka.
Sijajua majaji wa Tanzania wana ugomvi gani na mimi, au Chama cha ngumi kina ugomvi gani na mimi.
Napenda sana kumshukuru Mbunge, Sofia Mwakagenda kwa kuleta hili pambano, lakini chama cha ngumi hakinitendei haki.
Mchezo tumeuchukua kwasababu mzunguko wa kwanza hadi wa tatu tumempiga katompa, nadhani Mzunguko wa tano na wa sita ndio alipata alama yeye, lakini mzunguko wa mwisho wote tulikuwa tunabadilishana.
Sijajua Chama Cha Ngumi Tanzania kina nia gani na mimi.
Kama kuna ugomvi mimi wasinisamehe.
Dullah Mbabe akizungumza baada ya kupoteza pambano.
Ibrahim Class alikuwa spanning Partner na Second wa Dullah Mbabe hapo jana, baada ya Dullah kupoteza nae alielekeza lawama zake kwenye chama cha ngumi nchini Tanzania akidai kilipaswa kutoa upendeleo kwa bondia wa Tanzania kama ambavyo Mataifa mengine hufanya.
Sisi tunaenda Ulaya, tunashinda mechi vizuri lakini watu wanabeba uzalendo kwao.
Sisi tumeshinda vizuri, hii sio mechi ya kumfanya Dullah apigwe, hata chama cha ngumi huwa wanaona unaenda Ulaya unampiga mtu ana dondoka mara tatu au mara nne lakini ushindi anapewa bondia wao.
Vitu kama hivi vinaumiza watu tunaacha mambo mengine tunafanya kazi moja daah…
Kuna Usisi, tuache kuangalia mambo mengine ya mitandao, wenzetu Ulaya wanabebana sana…
Kama hawampendi Dullah wamwambie basi aachane na ngumi, inakuwaje Katompa anakuja hapa anapigana anapata ushindi wakati Dullah hajadondoka, kapata alama vizuri, wamepigana, halafu wanasema Dullah kapigwa, hakuna Usisi.
Chama cha ngumi kama wana ugomvi na Dullah wamsamehe, kwasababu sio sawa hakuna Utanzania.
Ibrahim Class, akizungumza baada ya pambano la Dullah na Katompa.
Rais wa Chama cha ngumi Tanzania Ndugu Chaurembo Palasa akasema amesikitishwa na kauli walizozitoa mabondia Dullah Mbabe na Ibrahim Clasa baada ya kupoteza pambano lao hapo jana.
Nimesikitishwa sana na kauli za Mabondia, ambao sio proffesional Boxing, watu wameona, wanadiliki kukishutumu Chama, mimi nafikiri labda zimewaruka akili zao kwasababu ngumi watu wameona na majaji wametoa point.
Kila mara mabondia hapa huwa wanacheza na huwa wanashinda, unaposema kwamba Chama cha ngumi hakihusiki na chochote, kwamba majaji wametoa point na ngumi zimeonekana.
Mimi nafikiri Bondia lazima ukubali matokeo, tuliona Twaha Kiduku alipigana hapa, lakini usishutumu Chama, ngumi ni mchezo kuna kushindwa na kushinda kwahiyo ukishindwa sio ajabu unajipanga unafanya tena.
Majaji ndio wameamua na watanzania wameona pambano, mimi nafikiri hizo shutuma hazina maana yoyote.
Chaurembo Palasa Rais TPBRC.
Mwandaaji wa pambano hilo Sophia mwakagenda (MB) amesema kama kuna bondia hajafurahishwa na matokeo hayo wanaweza kulirudia tena