CAF Champions League

JWANENG YASHUTUMIWA KUSHINDA KWA UCHAWI DHIDI YA WAC.

Published on

Kocha wa klabu ya Jwaneng Galaxy Morena Ramoreboli amevishutumu vyombo vya habari vya nchini Morocco kwa kusema kuwa Timu yake imetumia ‘UCHAWI’ kushinda mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad.

Kocha Ramoreboli ameomba timu yake iheshimiwe kwa kuwa ilikuwa na maandalizi mazuri ya mchezo.

Sasa unanishusha, unaniambia tumeshinda kwasababu ya uchawi aaah, acha kutukosea heshima, samahani hauwezi ukaongea namna hiyo.

Ramoreboli akijibu swali la mwandishi wa habari baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wydad Ugenini.

Baada ya kutoa majibu hayo komcha Ramoreboli akasimama na kuondoka kwenye mkutano na waandishi wa habari. Jwaneng jana iliishangaza Afrika baada ya kuifunga Wydad AC 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Mohamed V, Casablanca.

Mchezo unaofata kwa Jwaneng Galaxy ni dhidi ya Simba, mchezo ambao utapigwa nchini Botswana December 2 mwaka huu.

Popular Posts

Exit mobile version