CAF Champions League

SIMBA HALI MBAYA KIMATAIFA.

Published on

Klabu ya simba ya Tanzania msimu huu kwenye michuano ya kimataifa haijapàta ushindi wa aina yoyote katika michezo mitano (5) ya mashindano yote iliyoshiriki.

Imecheza michezo miwili ya michuano mipya ya African Football League dhidi ya Al Ahly na michezo yote ikitamatika kwa sare ya magoli, mchezo wa kwanza Dar Es Salaam na mchezo wa pili Cairo.

Simba 2-2 Al Ahly

Al Ahly 1-1 Simba.

Simba licha ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika lakini bado haijapata ushindi wowote na haijapoteza mchezo wowote hadi hivi sasa na imetoa sare michezo yote.

Power Dynamos 2-2 Simba

Simba 1-1 Power Dynamos

Simba 1-1 Asec Mimosas.

Mwenendo wa Simba iliyo chini ya kocha wa muda Daniel Cardena na Suleiman Matola msimu huu sio mzuri sana ukilinganisha na msimu uliopita.

Mchezo unaofuata kwa klabu ya Simba utakuwa dhidi ya Jwaneng Galaxy nchini Botswana December 2. Jwaneng inaongoza kundi kwasasa ikiwa na alama tatu (3) baada ya kuifunga Wydad AC goli 1-0 ikiwa ugenini nchini Morocco.

December 2,

16:00 Jwaneng Galaxy vs Simba.

Popular Posts

Exit mobile version