Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania [TFF], Wallace Karia mapema leo ameeleza mipango wanayoendelea kuitengeneza ili kuhakikisha uwanja wa Taifa [Benjamin Mkapa] unadumu kwa muda mrefu kwenye matumizi bila kuwa na changamoto yoyote.
Karia amesema moja ya vitu wanavyohitaji kuvifanya ni kuufanya uwanja huo uchezewe michezo miwili pekee ya Ligi kuu kwa mwaka, michezo inayozikutanisha klabu za Simba na Yanga huku wakiangalia uwezekano hata mechi za timu ya Taifa zihamishiwe uwanja mwingine.
Kwa upande mwingine pia Rais Karia ameeleza hali ya uwanja ulivyo kwasasa licha ya michezo mingi ya kimataifa kuchezwa hivi karibuni ikiwa pamoja na michezo ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika na michezo ya kufuzu fainali za kombe la Dunia 2026.
Juzi kulikuwa na mambo yanatakiwa yafanyike uwanja wa Taifa na yalikuwa yanahitaji hela nyingi na ndio kilikuwa kipaumbele chetu,uzinduzi wa African Football League AFL ,tukio la kihistoria linafanyika hapa,uwanja haukuharibika.
Wiki iliyopita kulikuwa na mechi tatu mfululizo ,Gambia vs Burundi ,Burundi vs Gabon ,Gambia vs Ivory Coast kisha Tanzania vs Morocco lakini uwanja bado ni mzuri tu.
Wiki hii Simba wamecheza hapo , Decenber 1, watacheza Al Hilal vs Esperance , December 2, Yanga vs Al Ahly na bado uwanja unasimama katika viwanja bora Afrika.
Wallace Karia, aliongeza.
Karia pia ametolea ufafanuzi juu ya taarifa zilizozagaa zikimhusisha yeye kumuingilia kocha katika zoezi la kuita wachezaji kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ huku ikizungumzwa kuwa yeye alihusika kwa kiwango kikubwa kumjumuisha Samatta kikosini licha ya mwalimu kutokumuita.
Kuita timu ni mwalimu ndio anaita ,kuna chombo kimezungumza kwamba mimi ndio naletewa majina ,nikaletewa majina Samatta hayupo nikamuingiza ,hakuna mwalimu ambaye atasimama na kusema TFF inamuitia timu.
Karia alizungumza.
Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa sasa unatumika kwaajili ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa klabu za Simba, Yanga zote za Tanzania na klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan iliyouchagua uwanja huu kuwa uwanja wake wa nyumbani.
Al Hilal itacheza December 1, huku Young Africans ikicheza December 2 katika uwanja huo huo wa Taifa [Benjamin Mkapa] Jijini Dar Es Salaam.