Hassan Mwakinyo ameondolewa adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja na Kamisheni ya kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC).
Bondia huyo alifungiwa mwaka mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni Moja kwa kushindwa kupanda ulingoni kwenye pambano lake la Septemba 29 dhidi ya Bondia kutoka Namibia, Julius Indongo.
Mwakinyo aligoma kuingia ulingoni akidai kuwa waandaaji wa pambano hilo walienda kinyume na makubaliano yao.