Boxing

SHINIKIZO LA VIONGOZI LATAJWA KESI YA MWAKINYO.

Published on

October 12, 2023 Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo alifungiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania [TPBRC] kucheza pambano lolote ndani na nje ya nchi kwa mwaka mmoja na kuhitajika kulipa faini ya Million Moja kwa kosa la kukataa kupanda ulingoni kwenye pambano la masumbwi lililopangwa kupigwa September 29, 2023 dhidi ya Julius Indongo.

Hata hivyo baada ya taarifa hiyo iliyotolewa na katibu wa TPBRC George Silas, Hassan Mwakinyo alilazimika kukata rufaa ili kuona kama anaweza kushinda kesi hiyo lakini rufaa yake haikusikilizwa. Sababu kuu za Mwakinyo kushindwa kupanda ulingoni alisema ni kukiukwa kwa makubaliano kati yake na kampuni ya promotion iliyokuwa imeandaa pambano hilo.

Baada ya ukimywa wa muda wa takribani mwezi mzima tangu taarifa za kufungiwa kwa Hassan Mwakinyo zitoke hatimae Jana, November 28, 2023, TPBRC imetoa taarifa ya kufunguliwa na kuruhusiwa kufanya mapambano kwa mara nyingine bondia huyo.

Rais wa TPBRC Chaurembo Palasa amesema kuwa Hassan Mwakinyo aliomba msamaha kwenye kikao hapo jana kilichohusishwa Baraza, Kamisheni na TPBRC na kikao hicho kwa pamoja kikatoa maridhiano ya kumsamehe bondia huyo na kumfungulia kwa mara nyingine tena.

Tulikuwa na kikao baina ya Baraza, TPBRC na kamisheni kwahiyo Hassan akawa ameomba msamaha kwenye kikao, kwahiyo tukakaa na kuona tumsamehe kwasababu mtu akishakiri kwamba alivyofanya si sawa kupanda ulingoni kwahiyo tukaona tumsamehe.

Ila tumetoa onyo kali kwake ili kwa siku nyingine au bondia mwingine asifanye/ asirudie kufanya hivyo.

Ili kuondoa migogoro kwenye tasnia yetu kwahiyo tukaona tumsamehe ili aendelee na kazi yake akiwa tu ataweza kutunza heshima maana wapenzi wa ngumi nao wanakasirika.

Sisi tumemsamehe lakini kuna watu wengine aliwafanyia makosa, kwahiyo yeye kama atakuwa na busara na hekima basi ataomba msamaha ili wamsamehe aweze kufanya shughuli zake kwasababu ngumi ni ajira.

Chaurembo Palasa, Rais wa TPBRC alizungumza.

Kwa upande wa waandaaji wa pambano hilo ambalo halikufanyika Godson Karingo baada ya taarifa hiyo kutoka akasema wanasikia taarifa kuwa kuna shinikizo kutoka mamlaka za juu walilopewa TPBRC ili wamfungulie Mwakinyo na wao wataendelea na kesi yao mahakamani.

Tunaambiwa kuna nguvu sijui shinikizo inatajwa kutoka kwa watu wakubwa, sisi tutaendelea kudai haki yetu hadi tutakapoona tumefikia mwisho.

Sisi tutachukua hatua ya kwenda Baraza kumuona Bwana Evod Kiando kumuuliza kumbe vikao vyako vilikuwa ni vya mtego, kwasababu hata kabla hatujafanya tekelezo tulilokubaliana msamaha umetoka na mtu kafunguliwa.

Kumbe walikuwa wanatuita pale kiini macho, kama kweli wao ndio wamefanya hivyo basi tutaenda kumuuliza lakini kama si yeye aliyefanya hivyo pia tutaviuliza vyombo vingine.

Godson Karingo, Promota wa pambano lililoahirishwa.

Popular Posts

Exit mobile version