CAF Champions League

SIMBA YABADILISHIWA UWANJA DHIDI YA JWANENG GALAXY.

Published on

Mchezo kati ya Jwaneng Galaxy na Simba wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya pili ambao awali ulipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Botswana, sasa utachezwa kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume mjini Francistown ambao ni kilometa 400 kutoka mji mkuu wa Gaborone.

Mechi hiyo itapigwa Jumamosi Desemba 2 saa 10 jioni, Simba itakuwa ikisaka pointi tatu baada ya kuanza na sare nyumbani huku Jwaneng ikiingia na morali baada ya kuchukua pointi tatu ugenini kwa Wydad Casablanca.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetaja sababu ya kufungia uwanja huo ni kutokidhi vigezo huku kikosi cha Simba kikitarajiwa kusafiri siku ya Ijumaa.

Popular Posts

Exit mobile version