African Football League

PITSO AHOJI USHIRIKI WA SIMBA AFL MBELE YA YANGA.

Published on

Kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly, Pisto Mosimane ameonyesha kutokuelewa vigezo vilivyotumika kwa timu kushiriki Ligi ya African Football League msimu huu.

Mosimane haelewi ni kwa namna gani Raja Casablanca na Zamalek hazikushiriki na kama kigezo ilikuwa ni kiwango, haelewi waliweza vipi kuiita Simba halafu wakaiacha Yanga.

Kuhusu African Football League bado sijui walitumia vigezo gani kuzipata timu nane shiriki, kama ni suala la kiwango na alama sioni sababu kwanini timu kama Raja Casablanca ama Zamalek kuachwa hizi nazitumia kama mfano tu.

Au unaziachaje Kaizer Chiefs ama Orlando, ni michuano ambayo agenda ilikuwa ni pesa na unaelewa hivyo, unaiita Simba halafu unaiachaje Yanga?

Pitso Mosimane, akizungumzia michuano ya AFL.

Michuano ya AFL imeanza kwa mara ya kwanza msimu huu ikishirikisha timu nane pekee kutoka pande zote za Afrika. Bingwa wa michuano hii ni Mamelodi Sundowns.

Hakuna kigezo rasmi kilichotumika ili kuzipata timu shiriki katika mashindano haya, na msimu ujao timu zinatarajiwa kuongezeka zaidi ya zile zilizoshiriki msimu huu.

Popular Posts

Exit mobile version