Kocha mkuu wa kikosi cha Young Africans, Miguel Gamondi ameonyesha kutokufurahishwa na maswala ya kutoa majina ya wachezaji kuelekea siku ya mchezo husika.
Yanga imekuwa na utaratibu wa kutoa majina kwenye siku ya mchezo wao wowote ule, walifanya hivyo kwenye michezo kadhaa iliyopita kwa kuita majina kadhaa kama Maxi day, Pacome day na Aziz Ki day.
Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly klabu ya Yanga imeitaja siku hiyo kuwa Bacca day, ikibeba maudhui ya mchezaji wao Ibrahim Hamad Abdullah Bacca.
Gamondi amesema kwa upande wake hafurahishwi na hali hiyo lakini kwasababu ni utaratibu wa kibiashara wa klabu hawezi kuubadilisha.
Sikubaliani kabisa na huu utaratibu wa kuita mchezo Jina la mchezaji kwa sababu mchezaji hayupo peke yake wapo timu.
Jambo muhimu kwangu ni timu sio mchezaji mmoja binafsi, ila naelewa ndio utaratibu wa timu kwa ajili ya kufanya marketing.
Kuwafanya mashabiki waje uwanjani na kuuelewa zaidi mchezo husika najua huo ndio utaratibu wa klabu kuhamasisha ila sio utaratibu mzuri kwangu mimi binafsi.
Miguel Gamondi,kocha wa Young Africans.