NBC Premier League

TAKWIMU ZA KMC VS MASHUJAA LEO.

Published on

Ligi kuu kandanda Tanzania Bara itaendelea leo kwa mchezo mmoja [1] kupigwa katika uwanja wa Uhuru, Jijini Dar Es Salaam.

Kinondoni Manispaa [KMC] ya Dar Es Salaam itashuka dimbani hii leo saa kumi Alasiri [16:00] kuikaribisha klabu ya Mashujaa ya mkoani Kigoma.

Kuelekekea katika mchezo huo, klabu ya KMC hivi karibuni imekuwa haina matokeo mazuri sana kama ambavyo Mashujaa pia haijapata matokeo mazuri kwenye michezo ya hivi karibuni.

Huu ni miongoni mwa michezo migumu zaidi kupigwa ndani ya Ligi kuu Tanzania Bara kutokana na timu zote mbili kutokuwa na matokeo ya kuridhisha.

TAKWIMU ZA TIMU HIZI MBILI KUELEKEA MECHI YA LEO.

  • KMC ipo nafasi ya tano [5] ya msimamo wa Ligi kuu ikiwa na alama kumi na sita [16], imecheza michezo kumi [10].
  • KMC imecheza michezo mitano [5] nyumbani, imekusanya alama kumi [10] na inashika nafasi ya tano [5] kwa timu zilizokusanya alama nyingi kwenye uwanja wake wa nyumbani.
  • KMC imeshinda michezo mitatu [3], imetoka sare mara moja [1], imepoteza mchezo mmoja [1], katika ardhi yake ya nyumbani msimu huu.
  • KMC imefunga magoli sita [6] na imefungwa magoli manne [4] ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani msimu huu kwenye mechi tano zilizopita.
  • Hadi hivi sasa KMC imecheza michezo mitatu [3] pekee bila kuruhusu goli kati ya michezo kumi [10] iliyocheza.
  • KMC imeshinda michezo minne [4], imetoa sare michezo minne [4] na imefungwa michezo miwili [2].
  • KMC imefunga magoli kumi [10] na imefungwa magoli kumi na mbili [12].
  • Mashujaa imecheza michezo nane [8] na imekusanya alama nane [8] ipo nafasi ya kumi na tano [15] ya msimamo wa Ligi kati ya timu 16 hadi hivi sasa.
  • Mashujaa wamecheza michezo mitatu [3] nje ya nyumbani, haijapata ushindi, imetoa sare mchezo mmoja [1] na imepoteza michezo miwili [2], imevuna alama moja [1] pekee.
  • Mashunjaa wamefungwa magoli matatu [3], haijapata goli lolote ikiwa ugenini hadi hivi sasa.
  • Hadi hivi sasa Mashujaa imecheza michezo minne [4] bila kuruhusu goli kati ya michezo nane [8] iliyocheza.
  • Mashujaa imeshinda michezo miwili [2], imetoa sare michezo miwili [2] na imepoteza michezo minne [4].
  • Mashujaa imefunga magoli matano [5], imeruhusu magoli tisa [9].
  • Kwenye mechi tano [5] za mwisho KMC imeshinda mchezo mmoja [1], imetoka sare michezo mitatu [3] na imepoteza mchezo mmoja [1].
  • Katika michezo mitano [5] ya mwisho Mashujaa imetoka sare mchezo mmoja [1] na imepoteza michezo minne [4].

Timu hizi zinaenda kukutana kwa mara ya kwanza kwenye Ligi kuu kandanda Tanzania Bara, hazijawahi kukutana kwasababu Mashujaa ndio imepanda daraja msimu huu.

Huu utakuwa miongoni mwa michezo bora sana kuutazama, kila timu ikihitaji kupata ushindi ili kuamsha morali ya timu zao kuelekea michezo inayofuata.

Popular Posts

Exit mobile version