Klabu ya Simba inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imefunguliwa kufanya usajili na shirikisho la soka Duniani FIFA na shirikisho la soka Tanzania TFF baada ya kuilipa klabu ya Teungueth ya Senegal pesa ilizokuwa inadai.
Klabu ya Simba ilikuwa inadaiwa na Teungueth sehemu ya pesa kutoka kwenye mauzo ya mchezaji wao Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal aliyetimkia nchini Ufaransa.
Simba ilishindwa kuilipa klabu hiyo ndani ya siku 45 tangu walipoamuliwa kufanya hivyo na shirikisho la soka Duniani FIFA baada ya kushindwa kwenye kesi iliyofunguliwa na klabu ya Teungueth ya Senegal.
Mkataba wa Simba na Teungueth ya Senegal ulikuwa unaitaka Simba kuilipa klabu hiyo sehemu ya pesa kama watamuuza Sakho kwenda kwenye klabu yoyote ile.