PBZ Premier League

DJUMA IRAMBONA AFUTWA KAZI KMKM.

Published on

Klabu ya KMKM ya visiwani Zanzibar imetangaza kuachana na kocha wake mkuu Masoud Djuma Irambona baada ya kudumu klabuni hapo kwa miezi minne pekee.

Masoud raia wa Burundi ameiongoza KMKM katika michezo 13 ya Ligi kuu visiwani Zanzibar, imeshinda michezo saba [7], amepoteza michezo minne [4], na sare michezo miwili [2].

Masoud alipoteza pia mchezo wa ufunguzi wa Ligi [Ngao ya jamii] na michezo miwili [2] ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika.

Popular Posts

Exit mobile version