Sare ya 0-0 hapo jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC mzunguko wa 13 kati ya Prison dhidi ya Ihefu imeifanya Ihefu kufikisha siku 60 bila kupata matokeo ya ushindi kwenye mechi 8 mfululizo tangu iliipoichapa Yanga Octoba 4 mabao 2-1 katika Uwanja wa Highland Estate, jijini Mbeya.
Ihefu imekuwa haina mwendelezo mzuri baada ya kupata sare nne sawa na idadi ya mechi walizopoteza huku Kocha Basena akiwa amesimamia mechi saba tu tangu alipojiunga na timu hiyo Octoba 16.
Prisons amabayo ipo nafasi ya 13 ikiachana nafasi moja na Ihefu, imeshinda mechi mbili, kutoka sare tano, kupoteza mechi tano na huku ikiwa na pointi 11 katika mechi 12.