Beki wa kushoto wa Yanga SC Mkongomani Joyce Lomalisa Mutambala ataukosa mchezo wa tatu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Medeama ugenini Ijumaa ya Desemba 8 utakaochezwa katika uwanja wa Baba Yara nchini Ghana.
Joyce Lomalisa alishindwa kuendelea na mchezo kwenye mechi ya pili makundi baada kuonekana akiugulia maumivu ya mguu kwa kuchezewe rafu na Percy Tau wa Al Ahly katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Yanga imeanza safari leo kuelekea nchini Ghana kwaajili ya kuivaa Medeama katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya michuano hiyo ya klabu bingwa barani Afrika.