NBA

MILWAUKEE BUCKS YA MOTO SANA

Published on

Giannis Antentokounmpo ameendeleza balaa lake msimu huu baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi dhidi ya New York Knicks kwa jumla ya vikapu 146-122 kwenye mchezo wa NBA In-Season Tournament usiku wa kuamkia leo.

Bucks walionekana kuutawala mchezo wakiongoza kwenye robo zote za mchezo mpaka mchezo unamalizika licha ya Knicks kuanza vizuri robo mbili za mwanzo wakitoa upinzani mkubwa, Julius Randle akifunga vikapu takribani 40+ akifunga vikapu vingi zaidi kuliko yoyote kwenye mchezo mzima kwa timu zote mbili.

Lakini ushirikiano mkubwa wa timu ya Bucks hasa ikiongozwa na Giannis na Damian Lillard ambao jumla yao walifunga vikapu 63 nyingine zikichangiwa na akina Brooke Lopez, Malik Beasley na Khris Middleton kupelela msiba huo kwa Knicks.

Kwa matokeo hayo Bucks wanafikisha ushindi wao wa 15 msimu huu huku pia wakifuzu kucheza nusu fainali ya michuano hii ya IN-SEASON na watakutana na Indiana Pacers waliowatoa Boston Celtics kwa vikapu 122-112.

Kwingineko, LA Lakers nao wamefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali pia ya michuano hiyo baada ya kuwafunga Phoenix Suns ya Kevin Durant kwa vikapu 106 -103 kwenye mchezo uliokuwa mgumu na wa kusisimua huku wakigawana nyakati, pengine ni robo ya mwisho ndio iliyoamua mchezo.

Ni LeBron James, Austin Reaves na Anthony Davis ndio walikuwa nyota wa mchezo kwa Lakers wakifunga jumla ya vikapu 78. Licha ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa KD na Devin Bookees hasa robo ya 3 lakini Lakers walipambana kuhakikisha wanakata tiketi ya kucheza nusu fainali na sasa watakutana na New Orleans Pelicans, timu ya zamani ya Anthony Davis walioingia hatua hii baada ya kuwafunga Sacramento Kings vikapu 127-117

Michezo ya Nusu fainali inatarajiwa kupigwa siku ya Ijumaa tarehe 08 Disemba, 2023.

Popular Posts

Exit mobile version