Medeama ilipangwa na Remo Stars katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Medeama ikafuzu hatua ya kwanza ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare kwenye matokeo ya jumla ya mechi mbili.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Ghana, Medeama ilishinda [Medeama 1-0 Remo Stars] halafu ikapoteza ugenini [Remo Stars 1-0 Medeama] lakini Medeama ikashinda kwa penati na kusonga mbele.
Kwenye hatua ya kwanza Medeama ikakutana na Horoya, mchezo wa kwanza Medeama ilishinda ikiwa nyumbani [Medeama 3-1 Horoya]. Mchezo wa pili Horoya ikiwa nyumbani ikashinda [Horoya 2-1 Medeama], licha ya kupoteza ugenini Medema ikafuzu hatua ya makundi kwa faida ya goli la ugenini.
Kwenye mechi za hatua ya makundi Medeama ilipoteza mchezo wake wa kwanza nchini Misri dhidi ya Al Ahly [Al Ahly 3-0 Medeama]. Ukiachana na kupoteza Medeama walipambana sana, walianza kuruhusu goli kuanzia dakika ya 66!
Mchezo uliofuata ulikuwa dhidi ya Belouizdad, Medeama ikashinda [Medeama 2-1 Belouizdad] tena kwa kufanya comeback!
Ushindi wa Medeama dhidi ya Belouizdad ukazishtua timu nyingine kwenye kundi hilo na kuanza kuiona ni mshindani.