Klabu ya soka ya Singida FG Wametangaza kuutumia uwanja wa Black Rhino Academy uliopo Wilaya ya Karatu jijini Arusha kama uwanja wao wa nyumbani kipindi hiki ambacho uwanja wao wa CCM Liti upo kwenye ukarabati.
Taarifa kutoka Singida FG inasema kuwa
Tutautumia uwanja wa Black Rhino Academy mpaka pale Uwanja wa CCM Liti uliopo mjini Singida utakapokuwa tayari kwa matumizi
Singida FG wanatarajiwa kuutumia uwanka wao kwenye mchezo wao dhidi ya KMC Disemba 11 kwenye mchezo wa ligi kuu lakini pia dhidi ya Arusha City kwenye mchezo wa FA.