Taarifa za ndani kutoka shirikisho la soka Afrika zinasema kuwa kuanzia mechi zijazo za Klabu Bingwa na Shirikisho litachukua sampuli za damu na mikojo ili kubaini matumizi ya dawa za kusisimua na kuongeza nguvu .Hii inatokana na uwepo wa viashiria kwa baadhi ya timu na mienendo yao.
Shirikisho la soka katika Kila nchi mwanachama analazimika kuandaa eneo maalum kwa ajili ya zoezi husika pamoja na kuweka mazingira rafiki katika utekelezaji wake.
Kwa kawaida tume ya kuthibiti matumizi ya dawa michezoni huratibu na kuwapima wana michezo kwa kushtukiza mara baada ya mchezo kumalizika
Dawa hizo zinazotumika kwa kunywa au kwa njia ya mishipa, huweza kuingia katika mzunguko wa damu. Zipo aina zaidi ya mia mbili ( 200 ) zenye viambatanisho na vichochezi vilivyopigwa marufuku kutumiwa kutokana na madhara yake kiafya na kunyima ushindani linganifu.
Anabolic steroids nazo zimezuiwa pamoja na jamii nyingine ambazo zina majina tofauti kibiashara. Dawa hizi hutengenezwa na wanasayansi kwa ajili ya tiba ila wasio na nia njema hutumia kwa uraibu au katika michezo.Zipo dawa (steroids ) zinatambulika na zinazokubalika kisheria za michezo kimataifa ilimradi hazimuongezei nguvu au kunenepesha misuli
Athari za matumizi kama ilivyoelezwa awali ni kubwa na za muda mrefu ikiwamo udumavu wa viungo , kubadilika maumbile , maumivu sugu, damu kuganda na mengi kisaikolojia
Duru za soka katika mashindano zinatawaliwa na mambo mengi ikiwamo imani za ushirikina. Timu ya Wydad imewasilisha malalamiko rasmi kwa shirikisho la soka Afrika Kwa vitendo vilivyofanywa na timu ya na Jwaneng Galaxy F.C. Zaidi kuna baadhi ya timu zimeonekana wakikabidhi wanyama hadharani ili wafanyiwe kafara kupata ushindi.