Makala Nyingine

JOHN BOCCO NDIO BASI TENA SIMBA SC.

Published on

Safari ya misimu saba ndani ya Simba kwa mshambuliaji John Bocco inakaribia ukingoni baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtoa kwenye mipango yao ya msimu ujao.

Simba sasa inajiandaa kuachana na wachezaji wake wasiopungua watano kwenye dirisha dogo hili la usajili huku wengine wakisubiriwa mwisho wa msimu ufike wamalize mikataba yao na kuondoka huru.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Dauda Sports, uongozi wa Simba tayari umemalizana na Bocco kwa kumpa uhuru wa kuchagua kuondoka Msimbazi kwenye dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kama ikishindikana basi atasubiri hadi mwisho wa msimu mkataba wake umalizike aondoke.

Hatua hiyo inakuja mara baada ya viongozi kukaa kikao cha maridhiano ya mabadiliko kwa wachezaji wa kutoka na kuleta maingizo mapya ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao, ambapo John Bocco akiwa ameridhia kuondoka katika klabu hiyo kwa kuthamini na kutambua malengo ya klabu kutoendana na kasi yake sababu ya umri wake kumtupa mkono

Popular Posts

Exit mobile version