CAF Champions League

KOCHA SIMBA, MAYELE SAFI, YANGA “OUT” TUZO AFRIKA.

Published on

Kocha Mkuu wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC Abdelhak Benchikha ni miongoni mwa majina matatu ya makocha Afrika wanaowania tuzo ya kocha bora.

Kocha huyo aliyejiunga na Simba SC hivi karibuni ameingia tatu bora ya kuwania tuzo hiyo akiwa na makocha Walid Regragui wa Morocco na Aliou Cisse wa Senegal.

Benchikha raia wa Algeria aliisaidia timu ya USM Alger ya Algeria kushinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kushinda kikombe cha Super Cup.

Shirikisho la Soka Afrika CAF wametoa orodha ya mwisho ya makocha hao, huku jina la kocha huyo wa Simba SC nalo likiwepo.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele jina lake limechomoza katika majina ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.

Mayele raia wa Congo amejiunga na timu hiyo baada ya kuwa na msimu mzuri na klabu ya Yanga SC msimu uliopita kwa kuisaidia timu hiyo kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho na kuibuka mfungaji bora katika mashindano hayo.

Nyota wengine wanaowania tuzo hiyo na Mayele ni Percy Tau wa Al Ahly ya Misri na Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Huku pia klabu ya Yanga SC imetupwa nje, kwenye kinyang’anyiro cha kuwania KLABU BORA YA MWAKA YA CAF huku zikibakia timu 3 za mwisho. Yanga iliyoingia 5 bora imeshindwa kuchomoza kwenye 3 bora ambako vilabu vya Wydad, Ahly na Mamelodi vimepenya katika hatua hiyo.

Popular Posts

Exit mobile version