EPL

RASHFORD BADO ANAJITAFUTA MAN UTD.

Published on

Nyota wa timu ya Taifa ya Uingereza Marcus Rashford aliwekwa benchi hapo jana kwenye Uwanja wa Old Trafford wakati timu yake ya Manchester United ilipoikaribisha Chelsea FC. Mashetani Wekundu walionyesha mchezo mzuri. Baada ya matukio ya wiki iliyopita, Erik ten Hag alihitaji sana mabadiliko ya kiuchezaji kutoka kwa timu yake dhidi ya Chelsea.

Kwa kuzingatia hilo, na taarifa za kutokuwa na furaha ndani ya kikosi cha United zikianza kuvuma, ushindi wa mabao 2-1 walioupata Jumatano kwenye Uwanja wa Old Trafford ulikuwa ni ishara tosha kwamba wachezaji wengi wa Ten Hag wamebaki nyuma ya bosi huku United wakitawala kwa takribani mechi nzima na kuwalazimisha wageni wao kufanya makosa mengi na kutumia makosa hayo kupata matokeo.

Scott McTominay alikuwa shujaa usiku huo huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland akifunga mabao mawili (2) huku lile la Chelsea likifungwa na Cole Palmer. Vijana wa Ten Hag walifanya vyema kwenye kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi nyingi nzuri, huku mlinda mlango wa Chelsea Robert Sanchez akiwa mmoja wa wachezaji wachache wanaorejea Magharibi mwa jiji la London akiwa kifua mbele kwa kuonesha mchezo mzuri baada ya kuokoa michomo mingi ambayo pengine kungeifanya Manchester United kuondoka na idadi kubwa ya mabao.

Soka la kasi na nguvu lililochezwa hapo jana lilionekana kutoendana na kasi ya mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford baada ya kuingia katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya Rasmus Hojlund kitu ambacho kinaonesha kuwa mshambuliaji huyo anaweza kupata wakati mgumu kulazimisha kurudi kwenye mipango ya kocha Eric Ten Hag.

Rashford hakuwa mshambulizi pekee wa England kuwa na siku mbaya kazini, kwani Raheem Sterling alikuwa mmoja wa wachezaji kadhaa wa Chelsea ambao hawakucheza vizuri usiku huo, huku Mauricio Pochettino akionekana kukosa mbinu mbadala ya kuilazimisha United kurudi nyuma.

Popular Posts

Exit mobile version