Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Dkt. Damas ndumbaro amesema kuwa amepewa maelekezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Taifa Stars wahakikishe inacheza fainali za kombe la Dunia 2026 na 2030.
Waziri amesema Serikali kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF watakaa na kuweka mipango ya kuhakikisha maelekezo ya Mh. Rais yanatimia.
Mh Rais ametoa maelekezo anataka Tanzania icheze fainali za Kombe la Dunia 2026 na 2030.
Mimi kama Waziri mwenye dhamana nimeyapokea maelekezo hayo tutakaa na wenzangu Shirikisho,Bodi ya Ligi na wadau wengine kuona tunatekelezaje maelekezo hayo.
Dkt Damas Ndumbaro, Waziri wa sanaa, Utamaduni na Michezo.