CAF Champions League

YANGA YATOA MSAADA KWA WATOTO GHANA.

Published on

Klabu ya Yanga kupitia kwa Rais wake Eng. Hersi Said kwa kushirikiana na GSM Foundation leo wametoa msaada katika shule ya Ahmed Uwais Islamic Basic School iliyopo Kumasi nchini Ghana.

Msaada huo umeambatana na dua kutoka kwa watoto waliopokea msaada huo wakiitakia heri klabu hiyo kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Medeama.

Huu umekuwa ni utaratibu kwa klabu ya Yanga kutoa misaada pindi timu yao inaposafiri iwe ndani ama nje ya mipaka ya Tanzania tangu msimu uliopita.

Yanga ina kibarua kizito mbele ya Medeama leo saa moja usiku [19:00] katika uwanja wa Baba Yara uliopo katika Mji wa Kumasi nchini Ghana.

Mchezo wa Leo kwa Yanga ni mhimu zaidi kwani wanazisaka alama tatu mhimu baada ya kushindwa kuzipata katika michezo miwili iliyopita.

Popular Posts

Exit mobile version