Coastal Union wataangalia nyuma na kuiona mechi yao dhidi ya Geita Gold wakishinda kwa mabao 3-1 kama mchezo wao bora waliocheza kwa kiwango cha hali ya juu pengine kuliko mchezo wowote msimu huu kuelekea mechi yao ya leo dhidi ya Kagera Sugar.
Mangush hawajawa na nyakati Bora sana hivi karibuni lakini kama watacheza hata robo ya kiwango walichoonyesha dhidi ya Geita basi ushindi dhidi ya Kagera leo ni mkubwa sana.
Nafasi ya 12 na alama 13 wanaona mwanya wa kusongea hadi nafasi ya 8 kama watapata ushindi leo.
Kagera Sugar walitoa sare ya 1-1 dhidi ya KMC huku wakisawazishiwa wakati wakiwa kwenye uongozi kipindi cha pili na mchezo ambao ulionekana wangeweza kupata matokeo kirahisi.
Mecky Mexime amekuwa akipambana sana na safu yake ya ushambuliaji sana sana huku wakipoteza nafasi nyingi za wazi licha ya kuwa na washambuliaji wazoefu kama Obrey Chirwa, Cleophace Mkandala na Anuary Jabir lakini magoli yamekuwa yakifungwa sana na Viungo au walinzi.
Kwenye mechi 4 za hivi karibuni ni mchezo mmoja tu waliofunga Chirwa na Mkandala(2-1 dhidi ya Prisons) lakini zingine zote fowadi zimekuwa butu. Kama kuna namna yoyote Kagera wanahitaji ushindi kwenye michezo yao basi ni kurekebisha eneo hilo.
Wakiwa wote wana alama 13 kila mmoja anaiona nafasi ya kupata alama 3 muhimu hivyo kuufanya mchezo huu kuwa na msisimko wa aina yake.
Mchezo utapigwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani majira ya saa 1 jioni.
WA KUANGALIWA
COASTAL UNION: MAABAD MAABAD ; Mfungaji wa Bao la pili dhidi ya Geita Gold huku akiwa kwenye kiwango bora sana amekuwa mshambuliaji tegemeo kiongozi huku Greyson Gwalala, Lucas Kikoti na Ibrahim Ajibu wakimzunguka.
KAGERA SUGAR : OBREY CHIRWA ; Pamoja na kuwa kimya sana kwenye ufungaji hivi karibuni lakini bado ni mshambuliaji hatari na wa kuchungwa.