CAF Champions League

SIMBA YAAHIDI KUREJEA IMARA CAF CL.

Published on

Kocha mkuu wa kikosi cha Simba Abdelhak Benchikah amesema kile walichokipata katika mchezo wa jana dhidi ya Wydad AC kitawafanya wajiandae vyema kuelekea mchezo ujao wa marudiano.

Yote yaliyotokea hapa yatakwenda kutupa usahihi wa maandalizi mazuri ya mchezo ujao. Eneo tulilokuwa bora tutakwenda kuongeza ili kuimarika zaidi na kwenye mapungufu tutakwenda kuparekebisha.

Abdelhak Benchikha, Kocha mkuu Simba.

Simba itakutana na Wydad AC tena December 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam.

Simba inahitaji alama mhimu katika mchezo huo ili ifufue matumaini ya kifuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Simba hadi hivi sasa ina alama mbili [2] ikiwa nafasi ya mwisho ya msimamo wa Kundi B, linaloongozwa na Asec Mimosas yenye alama saba [7], Jwaneng Galaxy alama nne [4], Wydad AC alama [3].

Simba inahitaji alama tatu mhimu kwenye kila mchezo kwenye michezo mitatu iliyobakiza ili kupata uhakika wa kuendelea na mashindano haya.

Simba imebakiza michezo miwili nyumbani dhidi ya Wydad AC na Jwaneng Galaxy huku ikisalia na mchezo mmoja ugenini dhidi ya Asec Mimisas.

Popular Posts

Exit mobile version