CAF Champions League

BENCHIKHA ALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI

Published on

Kocha wa klabu ya soka ya Simba, Abdelhak Benchikha amelia na ubutu wa safu yake ya ushambuliaji baada ya kucheza takribani mechi 3 bila kufunga bao lolote(la mchezo wa nje sio Penati).

Benchikha aliyasema hayo baada ya kutua nchini wakitoka nchini Morocco

Naridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu kinavyokuwa siku hadi siku. Wananisikiliza mazoezini na wanajituma uwanjani. Walinzi wanakaba na kucheza kama ilivyo kwa viungo wangu pia lakini tatizo lipo kwenye safu yangu ya ushambuliaji. Hatujafunga dhidi ya Jwaneng wala Wydad na hata dhidi ya ASEC tulifunga bao la Penati. Tunahitaji kufanya kazi.

Aidha Mwalimu Benchikha hakusita kuzungumzia mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad AC na umuhimu wa mchezo huo.

Lazima tushinde mchezo huo hakuna namna nyingine kama kweli tunataka kusonga mbele. Tumewaona ni wazuri lakini na sisi ni bora pia. Tuna uwezo wa kushinda mchezo huo nyumbani lakini ni lazima washambuliaji wangu wafunge. Hatuwezi kushinda kama hatufungi magoli.

Simba wanatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kurejeana na Wydad AC Tarehe 19 Disemba 2023.

Popular Posts

Exit mobile version