NBC Premier League

LIGI KUU YA NBC, KUENDELEA HII LEO.

Published on

Utamu wa Ligi Kuu ya NBC unaendelea tena leo kwa mechi mbili zitakazopigwa viwanja viwili tofauti, huku macho na masikio yakielekezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex wakati vinara wa ligi hiyo, Azam na maafande wa JKT Tanzania zitakapovaana na kila upande ukipiga mkwara mzito moto utawaka Chamazi.

Azam na JKT zitacheza majira ya 1:00 usiku, lakini mapema jioni kwenye Uwanja wa Liti itapigwa mechi nyingine kati ya Singida Fountain Gate itakayoikaribisha KMC iliyotoka kupigwa mabaio 5-0 na Azam FC kwenye mchezo uliopita.

Rekodi zinaonesha mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana kwenye Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Oktoba 30, 2020 na kushindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1, Azam ikipata bao kupitia kwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambaye kwa sasa anaichezea Yanga huku lile la JKT likifungwa na Michael Aidan.

Hii ni mabeki wa JKT watakuwa na kazi ya kuwazuia washambuliaji wa Azam wanaoongozwa na Prince Dube, Idd Seleman ‘Nado’, Kipre Junior, Gjibril Sillah na Feisal Salum ambao wameonekana kuwa moto kwa mechi nne zilizopita wakifunga jumla ya mabao 16.

Popular Posts

Exit mobile version