Wauwaji wa Kusini Klabu ya Namungo Fc yenye makazi yake Ruangwa mkaoni Lindi, leo Desemba 13,2023 imethibitisha rasmi kuachana na aliyekuwa Kocha wake Mkuu bwana Denis Kitambi huku Uongozi wa Klabu hiyo ikishindwa kutoa sababu za kwanini wameamua kuachana na Kitambi
Huku taarifa za ndani kutoka klabu hiyo zikieleza kuwa Kitambi anahusishwa kwenda kuwatumikia wajukuu wa mbogo maji Ihefu Sc iliyoachana na kocha wake Moses Basena.