Kocha mpya wa Simba, Abdelhak Benchikha leo amepata ushindi wa kwanza tangu atue Msimbazi baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda 3-0, dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam..
Mabao ya Simba yamefungwa na Saido Ntibazonkiza kwa penati dakika ya 44, baaada ya kukosa mabao ya wazi zaidi ya matatu, Kiungo Sadio Kanoute dakika ya 75, akafunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha krosi ya kichwa iliyopigwa na Mohamed Hussein, Bocco akamalizia kufunga bao la tatu dakika ya 90.
Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha alama 22 na kupaa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya NBC ikiwa imecheza mechi tisa huku juu yake ikiwepo Yanga yenye pointi 24 baada ya mechi tisa na Kileleni ikiwepo Azam iliyo na alama 28 ilizovuna katika michezo 12.
Kagera imesalia nafasi ya 12 kwenye msimamo ikiwa na alama 13 baada ya michezo 12.