Top Story

DAUDA: WACHEZAJI WAZAWA HAWATHAMINIWI KAMA WAGENI.

Published on

Kwa miaka ya hivi karibuni Ligi ya Tanzania imekuwa maarufu sana Barani Afrika, wachezaji na makocha wa hadhi za juu kutoka mataifa mbalimbali wamekuwa wakija kujiunga na klabu zetu.

Umaarufu huu unatokana na kufanya vizuri kwa klabu zetu hasa za Simba na Yanga katika michuano ya kimataifa lakini pia uwekezaji uliowekwa kwenye usajili wa nyota wakubwa.

Timu zimekuwa zikisajili kwa gharama kubwa sana nyota kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kuja kuleta mabadiliko kwenye klabu zetu, jambo ambalo limekuwa likiwekewa mitazamo tofauti na baadhi ya nyota na makocha wazawa.

Mchambuzi wa soka nchini Shaffih Dauda ametoa maoni yake kwa kusema kuwa nyota wengi wanaotoka nje wanathaminiwa zaidi kuliko nyota wanaotoka ndani ya nchi licha ya kwamba mchezaji wa ndani anaweza kuwa na uwezo zaidi ya mchezaji anayetoka nje ya nchi.

Mchezaji akishatoka nje ya nchi thamani yake inakuwa kubwa, lakini ukiangalia anachotoa kulinganisha na mzawa ni kidogo.

Mchezaji mzawa wanamjali kawaida anaweza kupewa laki tatu [300,000/=] kama kodi ya nyumba lakini wa kigeni anapangishiwa nyumba [Appartment] ya dolla Elfu Moja [1,000] au Elfu moja miatano [1,500], mtoto wake analipiwa ada ya shule [School Fees] kwenye shule za kimataifa.

Lakini huku una mzawa ambaye hujali kuhusu familia yake, kitu ambacho unajali unamuona kama yeye unamsaidia.

Tukibadilika tukawa na mtazamo chanya, hata kwa wenzetu ambao sisi tunao, itatusaidia kuwaongezea uwezo na kuwafanya kuwa bora.

Lakini kama haupo tayari kuwekeza kwenye kutengeneza.

Shaffih Dauda, Mchambuzi wa soka nchini

Kwasasa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inaruhusu timu kusajili wacheza kumi na mbili [12] wa kigeni huku idadi ya wachezaji wanaobaki wanakuwa wazawa.

Popular Posts

Exit mobile version