Klabu ya Wydad AC ya nchini Morocco imemfuta kazi kocha wake mkuu Adil Ramzi baada ya kutokuwa na matokeo ya kuridhisha tangu alipopewa nafasi ya kukinoa kikosi hicho.
Adil alifika fainali ya michuano ya AFL na kupoteza katima mchezo wa marejeano dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Msimu huu kwenye Ligi ya mabingwa Barani Afrika ameiongoza timu hiyo katika michezo mitatu, akipoteza miwili na kushinda mmoja dhidi ya Simba.
Ikumbukwe mechi ijayo Wydad atakuwa kwa Mkapa kukabiriana na Mnyama, Simba siku ya Jumanne Disemba 19.