NBC Premier League

LIGI KUU KUANZA KUTUMIA V.A.R

Published on

Muda sio mrefu Tanzania inaweza kuanza kushughudia matumizi wa technolojia ya Video Assistance Referee (VAR) kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya mchakato wake kuendelea vizuri.

Hatua hiyo inakuja kufuatia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa na kutumika katika baadhi ya viwanja vitakavyokidhi vigezo vya shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA).

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema hayo kwenye mkutano mkuu wa TFF unaofanyika mkoani Iringa leo jumamosi tarehe 16.12.2022.

Rais Karia amesema kuja kwa VAR kutoka CAF ni muendelezo wa uhusiano mzuri na TFF na CAF na tayari wataalam wameingia jana kwa ajili ya kutoa mafunzo.

Karia ameongeza kwamba Kamati ya waamuzi kwa vile imepewa jukumu la usimamizi watasaidia katika mafunzo na uzuri mkufunzi wa waamuzi wa CAF, Leslie Liunda atakuwa mratibu wa hayo mafunzo.

Kuna uwezekano pia wa VAR kufungwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar amesema Karia.

Popular Posts

Exit mobile version